@magufulijp - Twitter Profile Analysis

Analysis of 200 tweets by Dr John Magufuli, from 10 Sep 2015 to 22 Feb 2021.

@magufulijp twitter profile photo

Dr John Magufuli

verified twitter profile @MagufuliJP

The Fifth President of The United Republic of Tanzania.


241 tweets
1,009,329 followers
0 favourites
<1 tweet per day
2015 since
8 following
397 listed
Tanzania location

Top Tweets by @magufulijp

Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimesikitishwa na kifo cha Prof. Benno Ndulu (Ex-Governor BOT). Pole kwa familia na wafiwa wote. Nitamkumbuka kwa ushauri wake wa kuimarisha uchumi wa nchi yetu hususani mageuzi ktk sekta ya fedha. Alikuwa mchapakazi na mnyenyekevu. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi,Amina
22 Feb, 2021 - 04:56 PM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. Natoa pole kwa Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Mwinyi, Familia, Wazanzibari, wanachama wa ACT-Wazalendo na Watanzania wote. Mungu amweke mahali pema peponi,Amina
17 Feb, 2021 - 10:04 AM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Kwa miaka 44 chama cha CCM kimeendelea kuongoza mapambano ya kulinda heshima na uhuru wa Tanzania, kazi iliyoasisiwa na vyama vya TANU na ASP. Hongereni Watanzania; Hongereni Waafrika
05 Feb, 2021 - 01:47 PM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nakupongeza Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kwa kutangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Uganda kuwa mshindi wa kiti cha Urais. Tanzania itaendeleza urafiki na udugu wetu kwa maslahi mapana ya wananchi. Hongereni Waganda kwa kukamilisha Uchaguzi Mkuu, endeleeni kudumisha amani na upendo.
16 Jan, 2021 - 04:34 PM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimesikitishwa na kifo cha Ndg. Subhash Patel. Wakati wa uhai wake ametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya viwanda, kukuza biashara na kuzalisha ajira kwa Watanzania wengi. Natoa pole kwa Familia, CTI, TPSF na TNBC ambako alishiriki vizuri. Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un.
16 Dec, 2020 - 06:43 PM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimesikitishwa na kifo cha Kamishna wa Maadili, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Harold Nsekela. Poleni familia, watumishi wote wa Sekretarieti ya Maadili na Mahakama. Jaji Mstaafu Nsekela alikuwa mwadilifu, mzalendo, asiyejikweza na mchapakazi. Mungu amweke mahali pema, Amina.
06 Dec, 2020 - 10:00 AM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
I am deeply saddened by the news about the passing on of the former President of Ghana, H.E. Jerry John Rawlings. My condolences to Your Excellency Nana Akufo-Addo and the brotherly people of Ghana for the loss of this Great-man of Africa. May his soul rest in peace, Amen.
12 Nov, 2020 - 05:37 PM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
On behalf of the Government and the people of Tanzania, I congratulate President-elect @JoeBiden and Vice President-elect @KamalaHarris on your victory in the US General Election. Be assured that Tanzania will continue to cherish the relationship that exist between our countries.
10 Nov, 2020 - 07:39 PM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Naitwa John Pombe Joseph Magufuli, mgombea kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Ewe Mtanzania mwenzangu, naomba kura yako ya ndio tarehe 28/10/2020. Chagua Magufuli kwa maendeleo ya kweli ili tuendelee kujenga Tanzania mpya. Asante.
15 Oct, 2020 - 08:24 PM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nawapongeza Walimu wenzangu wa madaraja yote kwa kuadhimisha siku ya Walimu Duniani. Serikali inatambua mchango wenu mkubwa kwa Taifa na itaendelea kuboresha maslahi na mazingira yenu ya kazi. Endeleeni kuchapa kazi. Tulianza pamoja, tutamaliza pamoja. : Mwl. John Pombe Magufuli.
05 Oct, 2020 - 01:50 PM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nawapa pole familia na wote walioguswa na kifo cha Jaji Mstaafu Mark Bomani. Nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa Serikalini katika masuala ya sheria na katika chama akiwa Mjumbe wa Baraza la Wadhamini wa CCM. Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina.
11 Sep, 2020 - 02:53 PM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nawashukuru wana CCM wote na Watanzania wa vyama vyote kwa kujitokeza katika uzinduzi wa kampeni za CCM 2020 Jijini Dodoma. Pia nawashukuru wasanii, waandishi wa habari, viongozi wa Dini, n.k waliojitokeza kuniunga mkono katika uzinduzi huu. Maendeleo hayana chama. Tanzania Hoyee
29 Aug, 2020 - 02:39 PM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
The Government and the people of Tanzania convey their warmest congratulations to Dr.Akinwumi Adesina on his re-election as the President of the @AfDB_Group. In our joint work over the last 5 years, we have appreciated your consistent commitment to Africa. HONGERA SANA πŸ‘πŸΌπŸ‘πŸΌπŸ‘πŸΌ
27 Aug, 2020 - 03:44 PM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha ghafla cha Rais wa Chama cha Wanamuziki wa Injili Tanzania, Dkt. Donald Kisanga aliyefariki dunia kwa ajali ya gari Jijini Dodoma. Mungu amweke mahali pema peponi, Amina.
10 Aug, 2020 - 05:42 PM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nawatakia heri WAKULIMA, WAFUGAJI na WAVUVI katika sikukuu hii ya Nanenane. Serikali inatambua mchango wenu mkubwa katika ujenzi wa Taifa na ustawi wa Watanzania. Tunaahidi kuendelea kuwaunga mkono na kushughulikia changamoto zenu ili kuongeza tija katika kazi zenu. NANENANE JUU!
08 Aug, 2020 - 02:17 PM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimesikitishwa na kifo cha Mzee wetu Benjamin Mkapa (Rais Mstaafu wa Awamu ya 3). Nitamkumbuka kwa mapenzi yake makubwa kwa Taifa, ucha Mungu, uchapakazi na utendaji wake katika kujenga uchumi. Hakika Taifa limepoteza nguzo imara. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina.
23 Jul, 2020 - 10:48 PM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimesikitishwa na kifo cha Mzee wetu Balozi (Mst) Job Lusinde. Nawapa pole Familia, wana Dodoma na Watanzania. Nitaukumbuka mchango wake mkubwa kwa Taifa akiwa Waziri, Balozi, Mdhamini wa CCM na Kiongozi wa Wazee wa Dodoma. Pumzika salama Mtani wangu, kazi kubwa umeifanya vizuri.
08 Jul, 2020 - 06:19 AM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Today, the World Bank has declared Tanzania Middle Income Country. In this regard, I congratulate all my compatriots for this historic achievement. We had envisaged to achieve this status by 2025 but,with strong determination, this has been possible in 2020. GOD BLESS TANZANIA.
01 Jul, 2020 - 04:09 PM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Benki ya Dunia leo tarehe 01 Julai, 2020 imeitangaza Tanzania kuingia UCHUMI WA KATI.Nawapongeza Watanzania wenzangu kwa mafanikio haya.Huu ni ushindi mkubwa na kazi kubwa tumeifanya, tulipanga kuingia uchumi wa kati ifikapo 2025 lakini tumefanikiwa 2020.MUNGU IBARIKI TANZANIA
01 Jul, 2020 - 03:15 PM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nakupongeza Dkt. Lazarus Chakwera kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Malawi. Kwa niaba ya Serikali na Watanzania wote naahidi kuendeleza uhusiano wetu wa kidugu, kirafiki na ujirani mwema hususani katika masuala ya uchumi na ustawi wa jamii. Hongera sana Mhe. Rais.
01 Jul, 2020 - 10:05 AM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimeshtushwa na taarifa za kifo cha Rais wa Burundi, Mhe. Pierre Nkurunziza. Nitamkumbuka kwa uongozi wake imara na juhudi zake za kupigania amani, maendeleo na kuruhusu demokrasia. Kwa niaba ya Serikali na Watanzania nawapa pole familia na Warundi wote. Mungu amweke mahali pema.
09 Jun, 2020 - 05:56 PM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nakupongeza Ndg. Evariste Ndayishimiye kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Burundi. Wananchi wa Burundi wameonesha imani kubwa kwako. Kwa niaba ya Serikali na Watanzania wote naahidi kuendeleza uhusiano mzuri kati yetu. Nawatakia Warundi wote amani na ujenzi bora wa Taifa lenu.
06 Jun, 2020 - 04:19 PM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Ndugu zangu Watanzania, kutokana na ugonjwa wa Corona, nawaomba tutumie siku 3 za kuanzia tarehe 17- 19 Aprili, 2020 {Ijumaa, Jumamosi na Jumapili} KUMUOMBA MWENYEZI MUNGU aliye muweza wa yote atuepushe na janga la ugonjwa huu. Tusali kwa kila mmoja kwa imani yake, atatusikia.
16 Apr, 2020 - 03:52 PM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nawapongeza Wanawake wote kwa kuadhimisha siku hii muhimu. Mchango wenu kwa familia,jamii na Taifa hauna mfano.Serikali ninayoiongoza itaendelea kuwathamini,kuwaheshimu na kujenga mazingira bora yatakayowawezesha kutekeleza majukumu yenu ipasavyo. #HappyInternationalWomensDay
08 Mar, 2020 - 09:12 AM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nawapongeza wanachama na wakereketwa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa chama chetu kutimiza miaka 43 tangu kuzaliwa. Tunaposherehekea siku hii muhimu kwa kazi tuendeleze misingi ya chama chetu, tusimamie utekelezaji wa Ilani na tudumishe amani, upendo na mshikamano. CCM HOYEE!
05 Feb, 2020 - 02:13 PM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Kwa niaba ya Serikali na Watanzania nakupa pole Mhe.Rais Uhuru Kenyatta na Wakenya wote kwa kuondokewa na Rais Mstaafu Daniel Toroitich arap Moi. Watanzania tutamkumbuka kwa uongozi wake mahiri, jitihada za kuimarisha uhusiano wetu na Kenya na kufufua Jumuiya ya Afrika Mashariki.
04 Feb, 2020 - 06:06 AM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
It is with deep sorrow that I received the news about the demise of the Leader of Oman Sultanate, Sultan Qaboos bin Said Al Said. During his leadership, our two nations enjoyed strong and close bilateral relations. We convey our profound condolences to all the people of Oman.
11 Jan, 2020 - 02:12 PM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Nimehuzunishwa na taarifa za kifo cha rafiki yangu Ali Mufuruki (Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Jukwaa la Wakurugenzi Watendaji wa Kampuni - CEOrt) Nitamkumbuka kwa uzalendo na mchango wake katika kukuza sekta ya biashara na ushauri kwa Serikali.Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un.
08 Dec, 2019 - 10:23 AM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Hongera sana Mhe. Rais Hage Geingob. Your re-election is clear testimony of the trust and confidence that Namibians have bestowed on you. I wish to assure you of our continued support to further strengthen the historical ties between our two brotherly countries.
02 Dec, 2019 - 05:50 AM UTC
Dr John Magufuli
@MagufuliJP
Mhe. Spika. Nakushukuru wewe na Wabunge kwa azimio la kunipongeza. Mmenitia moyo na kunipa nguvu zaidi ya kufanya kazi. Nami nawapongeza kwa kazi nzuri mnazofanya Bungeni na Majimboni kwenu. Mbarikiwe sana.Kwa niaba ya Serikali naahidi kuendelea kushirikiana na Bunge letu Tukufu.
16 Nov, 2019 - 06:39 AM UTC

Top Retweets by @magufulijp

Narendra Modi
@narendramodi
Congratulations to President-elect of Tanzania Dr John P Magufuli on his election victory today. Also, a very happy birthday to him.
29 Oct, 2015 - 03:37 PM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Our next Commander-in-Chief, Dr John Pombe Magufuli, the President-elect of The United Republic of Tanzania.
29 Oct, 2015 - 01:11 PM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
#TaarifaOktoba26 Tunawaomba wana-CCM watulie, wasiwe na hofu, wawe na subira hadi Tume imalize kazi yake.
26 Oct, 2015 - 03:12 PM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Uchaguzi ni siku 1. Tanzania ipo siku zote. Tutunze amani na tumtangulize Mungu. Yeye anajua yote. - Dkt @MagufuliJP
25 Oct, 2015 - 08:56 AM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Tumshukuru Mungu tumeifikia siku hii. Nimetimiza wajibu wangu, sote tupige kura, demokrasia iamue. - Dkt @MagufuliJP
25 Oct, 2015 - 08:37 AM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Dkt @MagufuliJP atapiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Magufuli, kijiji cha Rubambangwe, kata ya Muungano, jimbo la Chato.
25 Oct, 2015 - 03:23 AM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Leo Oktoba 24 2015, Dkt @MagufuliJP anafanya mkutano kuhitimisha kampeni toka uwanja wa CCM Kirumba, Jijini Mwanza.
24 Oct, 2015 - 09:25 AM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Ujumbe wa Mama Maria Nyerere kuhusu Jumapili, Oktoba 25, 2015: https://t.co/AW1022UB9W #UjumbeKutokaButiama #ChaguoLaWananchi
21 Oct, 2015 - 02:35 PM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Dkt @MagufuliJP akifanya sala fupi kwenye makaburi ya Babu & Bibi yake kijijini Katoma,njiani kuendelea na mikutano.
19 Oct, 2015 - 11:22 AM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Uwanja wa Furahisha, jimbo la Ilemela Mwanza. Dkt @MagufuliJP akizungumza na wananchi jioni ya leo. #UmojaNiUshindi
17 Oct, 2015 - 02:48 PM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Nitaunda Baraza la Mawaziri waadilifu, wawajibikaji, sio 'njoo kesho', 'tuko kwenye mkutano', tuko kwenye mchakato'.
15 Oct, 2015 - 05:25 PM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Leo saa 7 mchana Dkt @MagufuliJP ameshuhudia uwekaji sahihi wa ujenzi wa Flyover ya TAZARA. #HapaKaziTu
15 Oct, 2015 - 11:59 AM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Sihitaji utajiri, siutafuti. Miaka yote nimekuwa muadilifu na kumtanguliza Mungu katika kuwatumikia. Nitabaki kuwa hivyo. - Dkt @MagufuliJP
15 Oct, 2015 - 06:36 AM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Wataalamu hao wazalendo katika uchumi, biashara, utawala & sheria, wanatoka taasisi za elimu ya juu, asasi zisizo za kiraia & sekta binafsi.
11 Oct, 2015 - 01:03 PM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Dkt. Magufuli, ameunda jopo la wanataaluma na wataalamu huru magwiji kwa ajili ya maandalizi ya kufanya mabadiliko makubwa Serikalini.
11 Oct, 2015 - 12:56 PM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Mjini Moshi, Dkt @MagufuliJP amewapokea wanachama wa upinzani waliohamia CCM, wakiongozwa na Katibu wa Chadema jimbo la Hai, Jubilant Lema.
07 Oct, 2015 - 03:17 PM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Mazungumzo ya Dkt @MagufuliJP na wananchi Moshi leo yamegusia ajira, viwanda, utalii, miundombinu, afya, elimu, ardhi na umoja wa kitaifa.
07 Oct, 2015 - 03:15 PM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Mafisadi hata ndani ya CCM wapo, na inahitaji mtu ambaye ni shujaa kulisema hili. Mmeona wameanza kutoka nilipochaguliwa. - Dkt @MagufuliJP
07 Oct, 2015 - 10:51 AM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Kondoa tuliahidi barabara ya lami 261km, Babati-Dodoma. Nyote mmeona kazi hiyo inaelekea kukamilika. Tukiahidi, tunatimiza. -Dkt @MagufuliJP
04 Oct, 2015 - 10:57 AM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Asilimia mbili ya Watanzania ni wazee. Kuanzia mwaka 2016 tutaanza kuwapa pensheni ya kujikimu.- Dkt @MagufuliJP #TukiahidiTunatimiza
04 Oct, 2015 - 10:51 AM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Tusikabidhi nchi katika mikono ya mafisadi. Wataiuza. Watanzania bila kujali vyama nahitaji kura zenu, tuungane kwa maendeleo. - @MagufuliJP
02 Oct, 2015 - 01:00 PM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
2003, Singida haikuwa na hata 1km ya lami. Katika kipindi cha miaka 10 zimejengwa 474km za lami. Tutafanya zaidi ya haya. - @MagufuliJP
02 Oct, 2015 - 12:36 PM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Sehemu ya wananchi wa Dodoma mjini waliojitokeza kumsikiliza Dkt @MagufuliJP, uwanja wa Jamhuri. #UmojaNiUshindi
30 Sep, 2015 - 02:14 PM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Sehemu ya wananchi wa mji wa Iringa waliohudhuria mkutano wa Dkt @MagufuliJP katika uwanja wa CCM Samora. #HapaKaziTu
28 Sep, 2015 - 02:53 PM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Hatuwezi kukaa Shinyanga yenye ng’ombe bila kuwa na kiwanda cha nyama. Kiwanda kitawezesha Watanzania wengi kupata ajira. - @MagufuliJP
26 Sep, 2015 - 11:52 AM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Walikuja kuomba udhamini wakawahonga. Mimi sikuwahonga hata senti tano. Aliyeona unafaa kununuliwa, hatashindwa kukuuza. Dkt - @MagufuliJP
26 Sep, 2015 - 08:00 AM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Sehemu ya mkutano wa Dkt @MagufuliJP na wananchi mjini Geita siku ya leo, Septemba 23, 2015. #HapaKaziTu
23 Sep, 2015 - 06:47 PM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Pongezi kwa Sheikh Aboubakar Zuberi kwa kuchaguliwa kuwa Mufti Mkuu wa Tanzania. Mungu amjalie hekima na afya katika kutimiza majukumu yake.
11 Sep, 2015 - 06:21 AM UTC
Chama Cha Mapinduzi
@ccm_tanzania
Jeshi la Kujenga Taifa, Makutopora mwaka 1983. @MagufuliJP akiwa na miaka 24, katika mafunzo ya kijeshi. #HapaKaziTu
10 Sep, 2015 - 05:46 PM UTC
January Makamba
@JMakamba
Yesterday I had the pleasure of welcoming @MagufuliJP, the next President of Tanzania, in my constituency.
10 Sep, 2015 - 06:57 AM UTC

@magufulijp's

Tweets

170 tweets
30 retweets
0 replies
@magufulijp's

Twitter Client

100 Twitter Web App
93 Twitter Web Client
6 Twitter for iPhone
1 Twitter for Android
@magufulijp's

Tweet Times

@magufulijp's

Tweet Days


@magufulijp's

Retweets

28 - ccm_tanzania
1 - JMakamba
1 - narendramodi
@magufulijp's

Replies

No replies found.
@magufulijp's

Hashtags

1 - #HappyInternationalWomensDay
@magufulijp's

Mentions

1 - @UKenyatta
1 - KagutaMuseveni
1 - AfDB_Group
1 - KamalaHarris
1 - JoeBiden